Serikali Yazifunga akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa Korosho Kupisha Uhakiki - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, December 29, 2018

Serikali Yazifunga akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa Korosho Kupisha Uhakiki“Wakulima 100,534 wameshalipwa bila kujali ni mara ngapi walipeleka korosho kwenye chama cha ushirika cha msingi. Wakulima hawa wanatoka katika vyama vya msingi 398 kati ya vyama 617 vilivyosajiliwa nchini na vyama 504 vinavyopatikana katika mikoa mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma,” alisema. Alisema tani 188,799. 4 za zao hilo zimeshakusanywa katika maghala mbalimbali na kwamba tani 30,226.25 zimehamishiwa kwenye maghala mengine ili kutengeneza nafasi korosho zilizo mikononi mwa wakulima kupokewa. 

Takwimu za Serikali zinamaanisha kuwa Sh206.092 bilioni zilizotolewa ni malipo kwa tani 62,452.333 kati ya tani 188,799 zilizokusanywa na tani 126, 347.07 zinasubiri mchakato wa malipo. 

“Mchakato hautakamilika mwisho wa mwezi huu kama tulivyotarajia kutokana na changamoto zilizojitokeza, matumaini yetu ni kwamba uhakiki na malipo yatakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.”

Credit:Mwananchi
Loading...

No comments: