SIMBA YAITANDIKA NKANA 3-1 TAIFA NA KUIFUNGASHIA VIRAGO MASHINDANO CAF


Mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza kuwania kufunzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Nkana FC ya Zambia imemalizika kwa Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Dakika 5 za mwanzo Simba walianza vizuri ila ndani ya dakika 15 walipoteana na kuruhusu bao la dakika ya 16 lililofungwa na Walter Bwalya baada ya kushambulia lango la Simba kwa muda mrefu.

Iliwalazimu Simba wasubiri mpaka dakika ya 29 akimalizia pasi ya Claytous Chama na dakika ya 45  Meddie Kagere aliandika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya  James Kotei.

Kipindi cha pili dakika ya 88 Claytous Chama alifunga bao akimalizia pasi ya Hassan Dilunga. 

Simba wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3.


8

Post a Comment

0 Comments