Sir Alex Ferguson kutua viwanja vya mazoezi vya Carrington kuungana na Ole Gunnar Solskjaer - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 30, 2018

Sir Alex Ferguson kutua viwanja vya mazoezi vya Carrington kuungana na Ole Gunnar Solskjaer


Aliyekuwa kocha wa klabu ya Manchester United mwenye mafanikio makubwa, Sir Alex Ferguson hii leo anatarajiwa kuwepo kwenye viunga vya Carrington kumpa ushirikiano meneja wa sasa Ole Gunnar Solskjaer ambaye ndiye aliyemualika.
Ferguson atakuwa na furaha kubwa atakapomuona Solskjaer pamoja na benchi lake la ufundi kwenye viwanja hivyo vya mazoezi vya Carrington wakati United ikijiandaa kuwakabili Bournemouth siku ya Jumapili kwenye uwanjawa Old Trafford.
Inaaminika kuwa Sir Alex Ferguson ndiye aliyempendekeza kocha Solskjaer kuja kuifundisha United hadi mwisho wa msimu akitokea Molde huku akiwa sambamba na Mike Phelan.
Image result for Sir alex ferguson
Straika huyo wa zamani wa United amejifunza vingi kutoka kwa Ferguson wakati alipokuwa akiitumikia timu hiyo.
Marakadhaa amekuwa wazi juu ya matamanio yake ya kurudisha soka la kushambulia zaidi ikiwa ni pamoja na tamaduni za United pamoja na kukuza vipaji vya vijana wadogo kutoka kwenye academy.
‘’Nilikuwa na mwalimu mzuri, siku zote alikuwa bora kwa hiyo utawala wangu utakwenda sambamba na vile nilivyojifunza kutoka kwake,’’ amesema Ole Gunnar Solskjaer.
Image result for Sir alex ferguson
Hii si mara ya kwanza kwa kocha huyo kualikwa itakumbukwa hata, Jose Mourinho aliwahi kufanya hivyo lakini Ferguson alishindwa kuhudhuria kwenye viwanja hivyo vya Carrington kufuatia kufanyiwa upasuaji wa ubongo.
Loading...

No comments: