STARS KUKUTANA NA WAKINA SALAH MISRI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 30, 2018

STARS KUKUTANA NA WAKINA SALAH MISRIKuna kila dalili kwamba Taifa Stars ikimfunga Uganda Machi 3 mwakani, itafuzu kwa fainali za Afcon ambazo zina nafasi kubwa ya kufanyika Misri badala ya Morocco na Afrika Kusini. 

Stars inahitaji ushindi kwenye mchezo huo huku ikiombea Cape Verde atoke sare na Lesotho nyumbani au kushinda mechi hiyo.

Habari za uhakika zinaeleza kuwa, Januari 9 Misri ana nafasi kubwa ya kutangazwa kuwa mwenyeji wa Afcon baada ya Cameroon kupigwa chini.

Ingawa Afrika Kusini nao wanawania nafasi ya kuandaa fainali hizo sawa na Morocco lakini Misri inapewa nafasi kubwa mpaka sasa kwakile kilichoelezwa kwamba miundombinu yao ipo tayari. Mmoja wa vigogo wa CAF.

Amaju Pinnick alisema watazingatia kigezo cha nchi iliyo tayari kimiundombinu kwavile muda uliobaki ni mchache.
Loading...

No comments: