Tsunami yaua watu 168 Indonesia, wengine wakutwa wakitumbuiza kwenye show jukwaani (+video) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, December 24, 2018

Tsunami yaua watu 168 Indonesia, wengine wakutwa wakitumbuiza kwenye show jukwaani (+video)


Watu 168 mpaka sasa wameripotiwa kupoteza maisha huku 750 wakijeruhiwa vibaya nchini Indonesia baada ya Tsunami kuikumba nchi hiyo siku ya jana usiku.
The wave hit beaches on the Sunda Strait - between the islands of Java and Sumatra (pictured residents inspect the damage to their homes on Carita Beach, Banten)

Mamlaka nchini humo zinasema Tsunami hiyo imetokea katika fukwe za visiwa vya Java na imesababishwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mlipuko wa volkano. 
Msemaji wa Taasisi inayoshughulika na kuzuia majanga nchini humo, Sutopo Purwo Nugroho amesema mpaka sasa watu 30 hawajulikani walipo, huku nyumba 558, migahawa 60 na ikibomolewa na Tsunami.
The killer wave was believed to have been caused by a volcanic eruption on nearby Krakatoa

Nugroho amesema tukio hilo ni la kushtukiza, kwani hakukuwa na taarifa wala tahadhari yoyote ile iliyotolewa kwa wananchi.
It is believed the tsunami was caused by an undersea landslide following the eruption of the Krakatoa volcano. The wave hit beaches on the Sunda Strait - between the islands of Java and Sumatra (pictured damaged buildings in Carita Beach, Banten province)

Usiku wa Jumamosi siku ya tukio, Bendi ya muziki maarufu nchini humo ya Band Seventeen, ikiongozwa na msanii wa muziki, Riefian Fajarsyah nayo ilipatwa na kazia baada ya jukwaa lao kufunikwa na maji.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Riefian Fajarsyah amethibitisha kuwa watu wanne kutoka kwenye bendi yake wamefariki dunia.
Mwezi kama huu mwaka 2004, tsunami kama hiyo ilitokea katika bahari ya Hindi kufuatia tetemeko la ardhi iliua zaidi ya watu 226,000 katika nchi 13 ikiwa 120,000 walikufa nchini Indonesia.
Loading...

No comments: