Wahamiaji haramu 13 wafariki baada ya kutelekezwa barabarani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 30, 2018

Wahamiaji haramu 13 wafariki baada ya kutelekezwa barabarani

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa  
Morogoro. Wahamiaji 13 kati ya 26 raia wa Ethiopia wamefariki dunia baada ya kutupwa eneo la Sangasanga mkoani Morogoro Barabara Kuu ya Iringa- Morogoro na gari aina ya lori ambalo halijajulikana.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Desemba 30, 2018, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo liliripotiwa saa 9 alasiri leo na Vyombo vya usalama kwenda eneo la tukio na kukuta raia 26 kati yao 13 wakiwa wamepoteza maisha.


Mutafungwa  amesema watumiaji wa barabara hiyo waliiona miili ya raia hao pembeni mwa barabara na kutoa taarifa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani eneo la Sangasanga.
Kamanda huyo amesema kati ya raia hao yumo mtoto wa miaka minane na polisi wanaendelea na uchunguzi ili kulibaini lori na wahusika wa tukio hilo.


MWANANCHI
Loading...

No comments: