Zahera: Boban safi, uwanja mbovu umempoteza! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 30, 2018

Zahera: Boban safi, uwanja mbovu umempoteza!

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema amefurahishwa na kiwango alichokionyesha kiungo wake mpya Haruna Moshi Boban na kuweka wazi kuwa alifanya kama alivyomuagiza.

Boban jana ulikuwa ni mchezo wake wa pili tangu amejiunga na timu hiyo akitokea African Lyon alianza na mchezo wa FA dhidi ya Tukuyu Stars ambapo alicheza dakika 26 huku timu yake ikifanikiwa kupata ushindi wa bao 4-0 na jana katika mchezo wa ligi na Mbeya City timu ikiibuka na ushindi wa bao 2-1.


Akizungumza na Mwanaspoti, Zahera alisema uwanja ndio uliomuaribia lakini alitoa pasi nyingi na kukaba kama alivyomwambia afanye kabla ya mchezo.

"Ni mchezaji mzuri na alicheza vizuri watu hawawezi wakamuelewa katika uwanja ule lakini naomba wampe muda watatambua ni kwanini nilitaka acheze katika kikosi changu kwasababu namuamini anauwezo na ataweza kuisaidia timu,"


"Pia wachezaji wenzake wakimjulia anacheza vipi basi watacheza vizuri na kuitengenezea matokeo mazuri timu ambayo inapambana kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika kila mchezo wanaocheza," alisema Zahera.


KWA HISANI YA MWANASPOTI

No comments: