20 WAUWAWA, 81 WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO NDANI YA KANISA KATOLIKI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

20 WAUWAWA, 81 WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO NDANI YA KANISA KATOLIKI


Watu takribani 20 wamefariki katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea jana Januari 27 katika Kanisa moja la Kikatoliki Kusini mwa nchi hiyo

Haijajulikana nani wako nyuma ya mashambulio hayo yaliyosababisha pia watu zaidi ya 81 kujeruhiwa

Mlipuko kwanza ulitokea ndani ya Kanisa Katoliki katika kisiwa cha Jolo huko Sulu wakati wa misa na mlipuko wa pili ukatokea katika uwanja yalikoegeshwa magari karibu na kanisa hilo

Haijulikani bado iwapo shambulio hilo ni matokeo ya kura ya maoni yanayolipatia utawala mkubwa zaidi wa ndani, jimbo hilo la Kusini wanakoishi jamii kubwa zaidi ya Waislam 

Majeruhi wakihudumiwa hospitali 

No comments: