AJIBU AIBUKA NA KALI JUU YA MKATABA WAKE NA YANGA, ANAONDOKA?


Nahodha wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema hawezi kuondoka ndani ya timu hiyo hivi sasa kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kuitimizia kile alichonacho, imeelezwa.

Ajibu ambaye alichukua kitambaa cha unahodha kutoka kwa Kelvin Yondani aliyevuliwa na Kocha Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa ni ngumu kuondoka kwake hivi sasa.

Mshambuliaji huyo ameibuka na kali kwa kusema hajui mkataba wake umebakiza muda gani lakini anachoangalia ni namna atakavyokuwa na wachezaji wenzake kama nahodha.

Aidha, taarifa imesema Ajibu ameeleza kuwa anacheza na wachezaji wenzake ndani ya Yanga hivyo itakuwa si rahisi kuwaacha kwa maana ana majukumu ya kuwaongoza kama Kapteni.

Wakati Ajibu akifunguka hayo, kikosi cha Yanga hivi sasa kipo katika maandalizi ya kucheza na Biashara kesho Jumamosi, mechi itakayokuwa ya Kombe la FA.

Post a Comment

0 Comments