ALIYETEMWA NA DIAMOND AIBUA MAKUCHA HADHARANI, AMCHANA VIBAYA MONDI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 10, 2019

ALIYETEMWA NA DIAMOND AIBUA MAKUCHA HADHARANI, AMCHANA VIBAYA MONDI


Mrembo ambaye anadaiwa kumwagwa na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ ameibuka na kulitolea povu penzi jipya la msanii huyo na mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna Barbier Okech ‘Zahara Zaire’. 

Kim ametoa povu hilo hivi karibuni mara baada ya Amani kumtaka azungumzie penzi jipya la Diamond ambaye awali iliaminika kuwa ndiye mumAewe mtarajiwa kabla jamaa huyo hajaibuka na Tanasha. Akimzungumzia zilipendwa wake huyo, Kim alisema mambo ya Diamond na Tanasha hayamhusu huku akielekeza lawama zote kwa mitandao ya kijamii.

“Hivi mnajua kiasi gani nimetukanwa kwenye mitandao ya kijamii? Na pia watu wa mitandao hawajui kabisa kufuatilia vitu kwa kina wanachojua ni kutukana watu lakini nashangazwa sana mimi kuhusishwa na Diamond, naomba kuweka wazi leo siko kwenye mapenzi na Diamond kwa sasa mimi nina maisha yangu na yeye hivyohivyo ndiyo maana amemuweka wazi mpenzi wake mpya kama ningekuwa ni mimi si angewaambia mashabiki zake kuwa ni mimi?” alisema Kim.

Baada ya kumwaga povu hilo, Amani lilimbana zaidi kuhusiana na ishu ya kubadilishwa dini na mama Diamond ambayo iliwahi kuripotiwa na gazeti hili mwishoni mwa mwaka jana. “Unajua hiyo ni sawa lakini siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja kwenye hilo kwa sababu anayeweza kuzungumza vizuri ni mama Diamond mwenyewe.” Hata hivyo Amani lilijaribu kumvutia waya mama Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ lakini simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa.

KIM ALIFIKAJE KWA DIAMOND?

Awali baada ya Diamond kumwagana na mama watoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mwanamitindo Hamisa Mobeto, alitajwa kubanjuka na muuza nyago Irene Hillary ‘Lynn’ ambapo uhusiano wao haukudumu, akahamishia majeshi kwa Kim Nana ambaye alionekana kukubalika na mama Diamond kabla Tanasha naye hajapindua matokeo kibabe ghafla.


CHANZO ; SALEHE JEMBE
Loading...

No comments: