ASKARI JWTZ AUWAWA AKIJIOKOA ASIBAKWE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

ASKARI JWTZ AUWAWA AKIJIOKOA ASIBAKWEJeshi la polisi mkoani Tabora linamshikilia Thomas Thobias kwa tuhuma za mauaji ya askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ)

Esther Gway, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ameuawa wakati akijinasua asibakwe na anayedaiwa kufanya kitendo hicho ni fundi ujenzi.

Fundi huyo inadaiwa alikuwa akijenga nyumba ya marehemu eneo la Kariakoo katika manispaa ya Tabora.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 28, 2019 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili Januari 27, 2019 saa moja usiku.

Kamanda Nley amesema kwamba mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake muda huo na kumkaba shingo kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka huku akimkaba shingoni alisababisha kifo chake. 

SOURCE: MWANANCHI 
Loading...

No comments: