BAADA YA KUIUA MAN CITY, BENITEZ ALETA MASHINE NYINGINE MPYAAA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

BAADA YA KUIUA MAN CITY, BENITEZ ALETA MASHINE NYINGINE MPYAAA
Klabu ya Newcastle United inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza leo wamekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Miguel Almiron akitokea Atlanta United FC kwa ada ambayo ni rekodi kwa klabu hiyo ya Pauni Milioni 21. 

Newcastle ambao wanapigania kutoka katika hatari ya kushuka daraja kwa msimu wa pili mfululizo wapo katika wakati mgumu kifedha hasa baada ya mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kuichoka na kutaka kuiuza klabu hiyo ingawa hakuna aliyejitokeza kutaka kuinunua. 

Usajili huu utamsaidia sana kocha Rafa Benitez ambaye amekuwa akiilazimisha klabu hiyo kusajili kwa muda mrefu bila mafanikio hadi akatishia kuondoka kama wasiposajili. 

Je unawaona Newcastle wakitoka katika Danger Zone na kufanya vizuri katika mechi zinazofuatia? Tupe maoni yako 
Loading...

No comments: