BAADA YA TAMASHA LA WASAFI NA KUFUNGULIWA KWAKE, DIAMOND ATUMA UJUMBE BASATA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, January 25, 2019

BAADA YA TAMASHA LA WASAFI NA KUFUNGULIWA KWAKE, DIAMOND ATUMA UJUMBE BASATA


Msanii anayefanya poa kwenye gemu ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema kwamba anamshukuru Mungu baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kumfungulia na kwamba amepata neema kubwa ikiwemo kuwa balozi rasmi wa Pepsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Ukumbi wa Serena Hotel uliopo Posta jijini Dar, wakati wa utambulisho wa kinywaji kipya cha Mkubwa Wao ambacho kilizinduliwa tangu Januari 21, mwaka huu, Diamond alisema mashabiki zake waendelee kuwa wavumilivu  kuhusu tamasha lao la Wasafi Festival kwani bado wanafikiria kama walianzishe upya au waendelee kufanya shoo mikoa iliyobakia, lakini kwakuwa tayari wameshafunguliwa basi hakuna shaka juu ya hilo watawajulisha kitachoendelea.

“Namshukuru  mwenyezi Mungu kwakuniweka hai na salama mpaka nafika hapa, lakini pia kabla yakuanza chochote pia niishukuru serikali yangu pendwa kwakunifungulia kifungo ambacho nilikuwa nacho, maana kifungo kinafunguliwa tu na neema hizo zinakuja.

“Niwashukuru watu wote ambao wameisapoti Wasafi Festival, nawashukuru sana kwa sababu mapokezi yalikuwa makubwa hatukuyategemea, lakini mimi na menejimenti yangu tulikuwa tunajadili tumalizie ile mikoa iliyobaki au tuanze na upya mwaka 2019, japo mzani unaelemea mwaka 2019 ili watu waliokuwa bado hususani mikoa ambayo hatujenda wawe na hamasa zaidi, hivyo tunawaomba mashabiki zetu wasichoke kutusapoti na kuendelea kuzifatilia kazi zetu nzuri,” alisema Diamond.

Diamond na Rayvanny walifungiwa na BASATA mwishoni mwa mwaka jana baada ya ku-perform wimbo wao wa Mwanza Nyegezi kwenye Tamasha lao la Wasafi Festival jijini Mwanza, wimbo ambao umefungiwa na Baraza hilo. Lakini juzi Baraza hilo lilitangaza kuwafungulia baada ya kuomba radhi.
Loading...

No comments: