BAADA YA USHINDI, KMC WAZIPIGIA HESABU KWA TIMU HII LIGI KUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 7, 2019

BAADA YA USHINDI, KMC WAZIPIGIA HESABU KWA TIMU HII LIGI KUUKIKOSI cha Halmashauri ya Kinondoni 'KMC' kimefanikiwa kuanza mzunguko wa pili kwa kishindo baada ya kufanikiwa kuvuna pointi tatu katika Uwanja Uhuru mbele ya JKT Tanzania.

KMC wamepata ushindi huo baada ya beki wa JKT Tanzania Ramadhan Madenge kujifunga dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza katika mchezo huo.

Ofisa Habari wa KMC Anwari Binde amesema kuwa ushindi huo unawafanya waanze kujiandaa kwa ajili mchezo ujao watakaocheza na Ruvu Shooting siku ya Ijumaa.

"Baada ya kumaliza mchezo ni wakati wetu kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu mwingine, muda wetu wa kufanya tathmini na kujua wapi tulikosea na kujua idadi ya majeruhi kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji walipata majeraha ili tuendelee kupambana," alisema.


CHANZO; SALEHE JEMBE
Loading...

No comments: