Benki zapewa jukumu kubadilisha fedha za kigeni, BoT yaonya dhidi ya maduka bubu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

Benki zapewa jukumu kubadilisha fedha za kigeni, BoT yaonya dhidi ya maduka bubu

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza kuwa kuanzia sasa huduma za kubadilishia fedha za kigeni zitapatikana kwenye benki na taasisi za fedha baada ya kusitisha huduma hiyo kupitia maduka ya kubadilishia fedha maarufu kama Bureau De Change.

Awali, Novemba mwaka jana BoT ilifanya ukaguzi kwenye maduka ya kubadilishia fedha Mkoani Arusha na kuyafungia baadhi ya maduka kutokana na kukiuka taratibu na sheria ikiwamo kukosa leseni za biashara hiyo.

Tarifa ya BoT iliyotolewa Alhamisi, Januari 31 imesema iliyafunga maduka hayo ili kupisha uchunguzi kwakuwa yamekuwa yakihusishwa na vitendo vya utakatishaji fedha.

BoT imezitaka benki na taasisi za fedha kutoa huduma hiyo kwa wateja wote wakati huu ambao uchunguzi unaendelea huku ikiwataka wananchi kuepuka kutumia maduka bubu.

                                                       

Loading...

No comments: