BOMBA LA MAFUTA: MAWAZIRI WA JPM, WA MUSEVENI WAKUTANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 26, 2019

BOMBA LA MAFUTA: MAWAZIRI WA JPM, WA MUSEVENI WAKUTANAWaziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wamefanya kikao kati yao na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
Kikao hicho kinachofanyika Kampala – Uganda ni cha maandalizi kabla ya kufanyika kikao na Mawaziri wa Uganda wanaohusika na mradi huo baadaye leo.
Kikao cha Mawaziri wa Tanzania na Uganda wanaohusika na mradi huo kinafanyika kufuatia majadiliano ya wataalam wa nchi hizi mbili yaliyoanza tarehe 21/1/2019 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazosimamia mradi kutoka Tanzania na Uganda kilichofanyika tarehe 24/1/2019.
Loading...

No comments: