Bomu lalipuka katikati ya jiji la Nairobi, hofu yatawala Kenya - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

Bomu lalipuka katikati ya jiji la Nairobi, hofu yatawala Kenya


Shambulizi la bomu limetekelezwa katikati ya jiji la Nairobi jana Jumamosi usiku na kujeruhi watu wawili, hii ni kwa mujibu wa polisi nchini humo.

Mashuhuda wanasema kuwa bomu hilo limelipuka katika eneo la Odeon, ambapo wamedai kuwa bomu hilo lilifichwa ndani ya begi na kutelekezwa kwenye mkokoteni.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi, Philip Ndolo akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa, bwana mmoja mwenye asili ya Kisomali alikodi mkokoteni huo na kupakia begi lake, na walipofika eneo la tukio, kwenye makutano ya barabara za Tom Mboya na Latema mmiliki huyo wa begi alitoweka.
Alimhadaa mwenye mkokoteni kwa kumwambia amsubiri akafuate kitambulisho chake ambacho alikisahau…hakurudi na baada ya muda mfupi kilipuzi kilichokuwamo ndani ya begi hilo kililipuka,“amesema Ndolo.
Shambulio hilo linakuja ikiwa ni wiki moja tu imepita tangu shambulizi la kigaidi la DusitD2 kutokea jijini Nairobi na kuuwa watu 21.
Bado hata hivyo, haijafahamika kama shambulizi hilo ni la kigaidi au laaah!
Loading...

No comments: