Chelsea Yamtaka Higuain

Straika Gonzalo Higuain

CHELSEA inasemekana inafanya mazungumzo na AC Milan ili wamchukue straika Gonzalo Higuain kwa mkopo.
Higuain anachezea kwa mkopo Milan, akitokea klabu yake ya Juventus. Ili kuwashawishi Milan inasemekana kuwa Chelsea ipo tayari kuwaachia Alvaro Morata. Hata hivyo, makubaliano baina ya pande hizo mbili lazime yapate baraka za Juventus.
Klabu hiyo inataka mbadala wa straika Morata, ambaye amechemsha kwenye Ligi Kuu England tangu ajiunge na Chelsea mwaka 2017 akitokea Real Madrid.
Chelsea ililipa ada ya pauni milioni 65 ili kumnyakua straika huyo, ambaye aliwahi kuchezea kwa mkopo Juventus.
Morata, 26, amefunga mabao saba tu kwenye mashindano tofauti msimu huu huku mabao matano yakiwa kwenye Ligi Kuu England.
Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri anataka kuongeza makali ya safu yake ya ushambuliaji na anaamini Higuain anaweza kufanya kazi nzuri.
Morata na mshambuliaji mwenzake Olivier Giroud hawako vizuri likija suala zima la kuifungia Chelsea.

Post a Comment

0 Comments