CHRIS BROWN ASHIKILIWA NA POLISI JIJINI PARIS KWA TUHUMA ZA UBAKAJI: - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

CHRIS BROWN ASHIKILIWA NA POLISI JIJINI PARIS KWA TUHUMA ZA UBAKAJI:Paris, France
Muimbaji wa muziki wa miondoko ya RnB, Mmarekani CHRIS BROWN pamoja na watu wengine wawili wanashikiliwa na polisi jijini Paris kwa tuhuma za ubakaji na masawa ya kulevya kutokana na msichana mmoja kufungua mashtaka juu yao.

Mshindi huyo wa Tuzo za Grammy, alikamatwa mnamo siku ya jumatatu kwa tuhuma hizo za ubakaji pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya na amebakia ndani leo jumanne na wachunguzi wana siku 2 zaidi za kuamua wamuachie au wamfungulie mashtaka mahakamani.

Maafisa habari wa lebo ya SONY MUSIC inayosimamia kazi za Chris Brown wamekataa kuongea chochote juu ya tuhuma hizo n ahata kusema Chris alikuwa anafanya nini jijini Paris. Pia mwanasheria wake Bwana Mark Geragos hakuweza kupatikana kwa haraka kuweza kusema lolote juu ya saga hii.

Kutokana na maelezo ya maafisa polisi wanasema Msichana huyo aliyefungua mashtaka alisema kuwa alikutana na Chris na wenzake wawili usiku wa tarehe 15 januari katika klabu iitwayo LE CRYSTAL na baada ya hapo walienda hoteli ya MANDARIN ORIENTAL iliyopo karibu na Concorde Plaza katikati mwa jiji la Paris. Inasemekana huko ndipo tukio lilipofanyika.

Mlinzi binafsi wa Chris Brown ni mmoja wa watu waliokamatwa pia na Uchunguzi bado unaendelea na lolote linaweza kutokea.

Loading...

No comments: