Christian Pulisic: Chelsea yamsaini mshambuliaji wa Dortmund kwa dau la £58m - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 3, 2019

Christian Pulisic: Chelsea yamsaini mshambuliaji wa Dortmund kwa dau la £58mKlabu ya Chelsea imemsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau la Yuro 64m lakini itamtoa kwa mkopo kwa klabu hiyo ya Ujerumani hadi mwisho wa msimu, 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Marekani , ambaye alikuwa amehusishwa na vilabu vya Liverpool na Arsenal , alijiunga na Dortumund akiwa mchezaji mchanga 2015. 
Pulisic amefunga magoli tisa katika mechi 23 akiichezea Marekani. 
''Ilikuwa ndoto ya Christian kujunga na ligi ya Uingereza'' , alisema mkurugenzi wa klabu ya Dortmund Michaek Zorc. 
Hiyo ni kutokana na mizizi yake ya Marekani na kutokana na hilo tulishindwa kuongeza mkataba wake.
''Na sasa tumekubali ombi zuri la Chelsea''. 
Kandarasi ya Pulisic katika klabu ya Dortmund ilitarajiwa kukamilika kufikia 2020.
Katika taarifa iliojaa hisia aliyochapisha katika mtandao wake wa Twitter, Pulisic alisema kuwa anaondoka Dortmund 'shingo upande'.
''Nahisi kama jana wakati nilipowasili katika klabu ya Dortmund, nikifurahia wakati nilipokuwa na umri wa miaka 16 kutoka mji mmoja mdogo wa Hershey nchini Marekani'', alisema. 
''Nisingalikuwepo hapa bila ya klabu hii na imani yao ya kuwapatia fursa wachezaji wachanga''.
''Kwa miezi sita ijayo, ni Dortmund pekee. tafadhalini musiwe na wasiwasi kuhusu upendo wangu , bidii na asilimia 110 ya kuichezea timu hii hadi nitakapopiga mpira wa mwisho msimu huu''.
'Ni mmoja ya wachezaji wachanga wanaosakwa Ulaya'
Pulisic alianza kuichezea klabu hiyo ya Bundelsiga akiwa na umri wa miaka 17 mnamo mwezi Januari 2016 na miezi miwili baadaye aliitwa kuichezea timu yake ya taifa. 
Amecheza mechi 81 katika ligi kuu ya Ujerumani na mechi 20 katika kombe la vilabu bingwa Ulaya. 
Amefunga magoli matatu katika mechi 18 katika mashindano yote msimu huu akiichezea Dortmund. 
Mkurugenzi mkuu wa Chelsea Marina Granovskai alimtaja Pulisic kuwa miongoni mwa wachezaji bora wanaotafutwa Ulaya.
''Akiwa na umri wa miaka 20 , tunaamini ana uwezo kuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa miaka mingi ijayo'', alisema. 
Mchezaji huyo ndio wa kwanza kusajiliwa na Chelsea tangu dirisha la uhamisho lifunguliwe tarehe mosi mwezi Januari. 
Ni mchezaji wa tatu anayelipwa pesa nyingi katika ligi ya Bundesliga, baada ya Ousmane Dembele aliyehamia Barcelona kutoka Dortmund kwa dau la £135m mwaka 2017 na dau la £55m alilonunuliwa Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg mwaka 2015.
Chelsea wako katika nafasi ya 4 katika ligi ya Premia, alama 11 nyuma ya Liverpool. 
Dortmund inaongoza katika jedwali la ligi ya Bundesliga kwa pointi sita na atakabiliana na Tottenham katika awamu ya mechi za kuingia robo fainali.


CHANZO; BBC
Loading...

No comments: