CRISTIANO RONALDO CHUPUCHUPU KWENDA JELA HISPANIA, ATOZWA FAINI KUBWA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

CRISTIANO RONALDO CHUPUCHUPU KWENDA JELA HISPANIA, ATOZWA FAINI KUBWA
Madrid, Spain
Straika wa klabu ya Juventus ya nchini ITALIA na mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, CRISTIANO RONALDO leo amenusurika kuishia jela baada ya kesi iliyokuwa ikimuandama ya ukwepaji wa kulipa kodi kutolewa hukumu leo hii katika mahakama kuu ya jiji la Madrid.

Mreno huyo ambaye alikuwa akiichezea klabu ya REAL MADRID tokea mwaka 2009 alipohamia kutokea klabu ya Manchester United, alikwepa kulipa kodi katika kipindi yupo katika klabu hiyo ya Madrid na baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na mamlaka za mapato za nchini Hispania ziligundua kuwa Ronaldo ameshiriki katika udanganyifu mkubwa wa kulipa kodi kat yam waka 2010 hadi 2014.

Katika hukumu iliyosomwa mapema leo, Ronaldo alitozwa faini ya paundi milioni 16.6 (Zaidi ya bilioni 40 za kitanzania) pamoja na kuhukumiwa miezi 23 jela. Lakini kwasababu sharia za nchi hiyo zinaruhusu mtu kutotumikia kifungo kama kipo chini ya miaka 2 (miezi 24) bwana Ronaldo amelipa faini tu na kuachiwa huru.

Ronaldo ambaye alikwenda jijini Madrid kuhudhuria kusikilizwa kwa kesi hiyo, aliambatana na mpenzi wake mwanamitindo Georgina Rodriguez huku wawili hao wakiwa kivutio kikubwa kwa waandishi wa habari na wananchi wa Madrid.Wachezaji wengine ambao wamewahi kukutwa na maswahiba haya ya kukwepa kodi nchini Hispania ni pamoja na mshindani wa Ronaldo, LIONEL MESSI, Xabi Alonso, Luca Modric, Marcelo Viera, Neymar, Ozil, Pamoja na kocha Jose Mourinho.

Loading...

No comments: