Darassa afunguka ishu ya kutumia madawa ya kulevya, kukaa kimya kwa muda mrefu na wimbo wake bora kwa mwaka 2018 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 26, 2019

Darassa afunguka ishu ya kutumia madawa ya kulevya, kukaa kimya kwa muda mrefu na wimbo wake bora kwa mwaka 2018


Image result for Darassa



Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Darassa amefungua kwa mara ya kwanza sakata la kutumia madawa ya kulevya kwa kusema kuwa hiyo ilikuwa ni skendo tu iliyotengenezwa na watu.
Darassa kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM amesema kuwa stori hizo zilitengenezwa kwa lengo la kuharibu Brand yake kwani walitaka kujua undani wa ukimya wake.
Sijui ni nani na sijui alitoa wapi? hizo stori zilikuja kwa lengo la kuja kuniharibu kisaikolojia. Lakini nilikuwa very Positive kuzi-handle,“amesema Darassa .
Darassa amesema kimya chake cha mwaka mmoja kwenye gemu, kilisababishwa na malezi ya mtoto wake na kujiandaa kimuziki zaidi ikiwemo kurekodi ngoma kila siku kwenye studio yake ya nyumbani.
Kwa upande mwingine, Darassa amesema kuwa wakati yupo kimya wimbo pekee uliomvutia zaidi ni wimbo wa Iokote wa Maua Sama .
Darassa amekaa kimya kwa miaka miwili bila kuachia ngoma wala kufanya Interview na Media yoyote hapa Tanzania na nje ya nchi.


BONGO5
Loading...

No comments: