Dhahabu Ya Mamilioni Ya Pesa Yakamatwa Ikitoroshwa Jijini MwanzaJeshi la Polisi Mkoani Mwanza limekamata kilo 323.6 za Dhahabu na fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni mia tatu na Milioni tano (305,000,000) jana  zikisafirishwa kuelekea mkoani Geita, ambapo watu watatu wanashikiliwa mpaka sasa kwa kosa la kusafirisha Dhahabu hizo kinyume na utaratibu.

Akizungumza baada ya kushuhudia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaonya Askari wasaliti au yeyote yule aliyeshiriki katika matukio hayo kwani ni sawa na msaliti wa nchi na kutoa maagizo kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha wahusika wote wanapatikana.Post a Comment

0 Comments