Diamond Afunguka Msanii Mpya Atakayetambulishwa WCB - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 19, 2019

Diamond Afunguka Msanii Mpya Atakayetambulishwa WCBMSANII nyota wa Bongo fleva, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka kuhusiana na kumsajili msanii wa kike katika lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).
Kupitia akaunti yake ya Tweeter January 18 msanii huyo aliandika: About to introduce a FEMALE Artist….. Coz i believe Women they can, if you Empower them….” (Nipo mbioni kumtambulisha msanii wa kike (WCB), kwa sababu naamini wanawake wanaweza, wakiwezeshwa)
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihisi nafasi hiyo huenda akaipata mwanadada Nandy ila Diamond mwenyewe hajathibitisha hilo.
Kubwa zaidi ni kuhusiana na ukaribu alionao Diamond na mwanamama Khadija Kopa, ambapo  kuna uwezekano mwanaye anayeitwa Zochu huenda akapata nafasi ya kusainiwa kwa sababu kwenye maneno yake kwenye Tweeter (wanawake wakiwezeshwa wanaweza) inaonekana msanii huyo bado ni mchanga na hajawahi kufanya ‘hit’.
Lebo ya WCB ina mwanamke mmoja ambaye ni Queen Darlin na wanaume  wanne (Lava Lava, Mbosso, Rayvanny na Harmonize)
Loading...

No comments: