Diamond PLATNUMZ Atoa Mpya..Aiomba Serikali Kutangaza 'Holiday' Akimuoa Tanash - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, January 27, 2019

Diamond PLATNUMZ Atoa Mpya..Aiomba Serikali Kutangaza 'Holiday' Akimuoa TanashMsanii wa Muziki, Diamond Platnumz amefunguka sababu za kupeleka mbele siku ya kumuoa mpenzi wake kutoka nchini Kenya.

Diamond katika siku yake ya kuoa ameiomba serikali imfanyie mpango iwe holiday kwasababu anataka siku yake hiyo iwe kubwa.

"Nilipeleka mbele siku kwasababu mzazi wa Natasha asingeweza kufika Valentine kwasababu anafanya kazi Belgium na likizo ilikuwa haipo hapo ukiacha hivyo sitaki harusi yangu iwe ndogo niichukulie poa poa tu, harusi yangu ikiwezekana hata serikali inifanyie mpango iwe holiday," alisema Diamond kwenye mahojiano yake na Mtanzania Digital.

Diamond wiki kadhaa alimpeleka mpenzi wake huyo nyumbano kwao kwenda kumtambulisha kwa familia yake.

Loading...

No comments: