Esma Afunguka Anavyomkubali Tanasha


DADA wa mwa­namuziki maarufu ndani na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan amefunguka kuwa ameshaanza kumpenda ‘kumoyo’ wifi yake mpya Tanasha Donna kiasi cha kujiuliza kwamba, mwana­dada huyo alikuwa wapi siku zote hizo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Esma alisema amekuwa na ukaribu kwa muda mfupi na wifi yake huyo lakini ametokea kumkubali na sasa ame­kaa kwenye moyo wake tofauti na alivyotarajia mwanzo kwani mtu akiwa mpya kumzoea inahitaji moyo kuridhia.
“Huwezi amini Tanasha tayari ameshakaa ndani ya moyo wangu, nampenda sana na kuna muda najiuliza alikuwa wapi muda wote? Kwa nini hakutokea mapema kwenye familia yetu? Hayo mambo ya kuniita Yuda hata siyajali kabisa, wata­jua wenyewe kwani mimi maisha yanasonga,” alisema Esma.

Post a Comment

0 Comments