Facebook kuunganisha WhatsApp, Instagram na Messenger - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

Facebook kuunganisha WhatsApp, Instagram na MessengerFacebook ina mipango ya kuunganisha huduma zake za kutuma ujumbe katika Instagram, WhatsApp na Facebook Messenger.

Licha ya kwamba huduma zote tatu zitasalia kuwa programu huru zitashirikiana kupitia ujumbe utakaotumwa kutoka huduma moja hadi nyingine, Facebook imeambia BBC kwamba ndio mwanzo wa mchakato mrefu.

Mpango huo kwanza uliripotiwa mjini New York na unaaminika kuwa mradi wa kibinafsi wa mwanzilishi wa facebook Mark Zuckerberg.

Utakapokamilika ushirikiano huo utamaanisha kwamba mtumiaji wa facebook anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye anamiliki akaunti ya WhatsApp, Hili haliwezekani kwa sasa kwa kuwa programu zilizopo hazina uhusiano.

Hatua ya kuunganisha huduma hizo tatu umeanza , kulingana na gazeti la The new York Times na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 ama mapema mwaka ujao.

Loading...

No comments: