Fid Q amshauri AY Alinunue Kontena Alilokuwa Akilala Dar - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, January 6, 2019

Fid Q amshauri AY Alinunue Kontena Alilokuwa Akilala Dar


Baada ya msanii wa Hip Hop Bongo AY' kuweka wazi alivyoanza harakati zake za muziki jijini Dar es salaam kwa kuishi kwenye Kontena, msanii mwenzake Fareed Kubanda maarufu Fid Q amemshauri alinunue Kontena hilo.

Fid Q ambaye bado yupo kwenye fungate la 'Honey Moon' baada ya kufunga ndoa wiki hii, amemshauri mkongwe mwenzake huyo alinunue Kontena hilo kisha atengeneze Studio kwaajili ya wasanii wanaotoka mikoani.

''Nimemshauri AY alinunue lile Kontena kisha aligeuze studio na kijiwe maalum kwa ajili ya wasanii wote wanaotoka mikoani na kuja dar Kwa ajili ya kuendeleza harakati zao za sanaa'', ameeleza Fid Q.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii AY ameweka wazi kuwa alikuja Dar es salaam mwaka 1999 kwaajili ya kuendeleza kipaji chake lakini hakuwa na pakufikia ikabidi awe analala kwenye Kontena moja maeneo ya Upanga.

No comments: