FIFA YAMFUNGIA MAISHA WAMBURA KUJIHUSISHA NA SOKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, January 23, 2019

FIFA YAMFUNGIA MAISHA WAMBURA KUJIHUSISHA NA SOKAKamati ya Nidhamu ya shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) imemfungia maisha MICHAEL RICHARD WAMBURA kujihusisha na mambo yote yahusuyo mpira wa miguu  (football related activities).

Katika uamuzi wake uliotolewa jana (Januari 22, 2019) na kutumwa shirikisho la soka Tanzania (TFF), kamati ya nidhamu ya FIFA chini ya mwenyekiti wake Ndugu Anin Yeboah wa Ghana, imekazia hukumu ya kamati ya rufani ya maadili ya TFF iliyotolewa April 6, 2018, hivyo, kutokana na kamati ya nidhamu ya FIFA kukazia hukunu ya kamati ya rufani ya maadili ya TFF, Ndugu Wambura ambaye alikuwa makamu wa raisi wa TFF hatakiwi kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu duniani kote.

TFF ambayo tayari imeshamkabidhi Wambura uamuzi huo, inawakumbusha wanafamilia wa mpira wa miguu kuzingatia maadili na nidhamu kwa kufuata taratibu zake kwa mujibu wa katiba za TFF, CAF na FIFA.

Barua iliyotolewa na TFF

Loading...

No comments: