Hakielimu yataja sababu za kuanguka kwa Shule za umma-matokeo Kidato cha nne - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, January 25, 2019

Hakielimu yataja sababu za kuanguka kwa Shule za umma-matokeo Kidato cha nne

                                Image result for Mkurugenzi Hakielimu


 
Dar es Salaam.Shirika la Hakielimu limetaja sababu za mwendelezo wa kuanguka kwa Shule za Umma katika matokeo ya Kidato cha nne huku likihimiza uboreshaji wa mfumo wa elimu ili kuzinusuru.

Katika matokeo ya Kidato cha nne ya mwaka 2018, umbapo ufaulu wake ulikuwa asilimia 78.3, Shule binafsi zimezidi kung’ara ikilinganishwa na zile za umma.

Aidha, Shule kongwe za vipaji maalumu zimeshindwa kuingia kwenye orodha ya kumi bora kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 na kutoa nafasi hiyo kwa shule binafsi kutamba.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Hakieimu, John Kalage amesema shule za umma zinakumbana na chanagmoto nyingi za kimazingira ambazo zimekuwa chanzo cha wanafunzi wengi kutofanya vizuri kwenye mitihani.

Kalage amesema kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17 inaonyesha shule za umma za Sekondari zina upungufu wa miundombinu kwa zaidi ya asilimia 50.

“Kumekuwa na changamoto kubwa ya mazingira ya kufundishia na kujifunzia.Unaweza kuangalia suala la uwiano wa walimu, uwezo wa walimu na suala la hamasa kwa walimu na miundombinu kwa ujumla,” amesema.

Alisema hata ufaulu wa masomo ya Hisabati, umekuwa chini ikichangiwa na uwezo hafifu wa walimu katika kufundisha masomo hayo.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mbali na shule za umma, ufaulu wa jumla kitaifa hauridhishi na kwamba ipo haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa juu ya namna sahihi ya kuboresha elimu nchini.

“Sisi kama Taifa lazima tuwekeze nguvu katika kubadilisha mfumo wetu wa elimu na kuhakikisha kwamba tunainua kiwango cha ubora wa elimu kwasababu haingii akilini kuona mtoto amesoma miaka minne halafu anatoka na sifuri,” amesema Kalage.

Katika matokeo ya mwaka 2018, shule zilizoingia kwenye kumi 10 bora ni St. Francis Girls, Kemebos, Marian Boys, Ahmes, Canossa, Maua Seminary, Precious Blood, Marian Girls, Bright Future Girls na Bethel Sabs Girls. Hakuna shule ya vipaji kama ilivyokuwa pia miaka ya 2015, 2016 na 2017.


Loading...

No comments: