Hakimu Ahoji Kesi ya Wema Sepetu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 29, 2019

Hakimu Ahoji Kesi ya Wema Sepetu


Baada ya Wakili wa Serikali, Mosia Kaima kudai kuwa kesi ya Muigizaji Wema Sepetu iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya kutajwa siku ya leo, upelelezi wake bado haujakamilika, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi wa kesi hiyo unakamilika kwa wakati

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

"Nataka upande wa mashtaka mkamilishe kwa wakati upelelezi ili kesi iweze kuendelea kwa sababu ni kesi ya muda mrefu tangu ifunguliwe mahakamani hapa Novemba mwaka jana na hadi sasa upelelezi bado?,” amehoji Kasonde.

Mbali na hayo Wakili wa Muigizaji huyo ameileza Mahakama kuwa kesi hiyo imeshatajwa mara nne mahakamani hapo huku upelelezi wake ukiwa bado haujakamilika.

"Naomba upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati kwa sababu shauri hili limeshatajwa kwa mara ya nne sasa, bila upelelezi wake kukamilika", amesema Wakili wa Utetezi.

Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 13, 2019 itakapotajwa tena na kuwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wao kwa wakati.

Wema alifikishwa kwa mara ya kwanza Kisutu, Novemba Mosi, 2018 kujibu shtaka la kuachapisha video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wa kijamii wa Instagram, kosa alilodaiwa kutenda Oktoba 15, 2018 .
Loading...

No comments: