JKT Queens Yaweka Rekodi ya Kipekee Ligi ya Wanawake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, January 20, 2019

JKT Queens Yaweka Rekodi ya Kipekee Ligi ya Wanawake


JKT Queens.
TIMU ya JKT Queens imeweka rekodi ya kipekee katika Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League baada ya kucheza michezo sita bila kpoteza hata mmoja.
Ligi Kuu ya Wanawake ambayo inashirikisha timu 12 mpaka sasa timu zote zimeshacheza michezo sita na zimefanikiwa kuweka rekodi yao ila JKT Queens mpaka sasa wamefanikiwa kuweka rekodi tamu.

Katika michezo sita wamefanikiwa kushinda michezo sita na kujikusanyia pointi 18 wakiwa ni vinara kwenye Ligi hiyo hawajaruhusu nyavu zao kutikishwa mpaka sasa na timu yoyote ile.

Yanga Princess ambao wamepanda daraja msimu huu wameanza vizuri kwani katika michezo sita waliyocheza mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo miwili na kujikusanyia pointi sita abazo zinawaweka nafasi ya saba tofauti na Evergreen Queens na Mapinduzi Queens ambao katika michezo sita hawajafanikiwa kushinda hata mchezo mmoja.
Simba Queens walikuwa wakipewa nafasi ya kumtungua JKT Queens wamebadilishiwa gia baada ya kucheza michezo sita wamepoteza mmoja na sare mchezo mmoja unaowafanya wajikusanyie pointi 13 nafasi ya tatu kwenye Ligi wakishushwa nafasi ya pili na Mlandizi Queens ambao hawajapoteza mchezo wana pointi 16.
Loading...

No comments: