KAMPUNI WASHIRIKA WA NAS (PLUTO TV) YAUZWA KWA MABILIONI YA PESA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

KAMPUNI WASHIRIKA WA NAS (PLUTO TV) YAUZWA KWA MABILIONI YA PESA


Kampuni ya Nas - Queensbridge Venture Partners Media Group ni washirika kibiashara na Pluto TV - moja ya televisheni kubwa za mtandaoni duniani.

Sasa taarifa njema leo ni kuwa Pluto TV imenunuliwa na kampuni nguli ya vyombo vya habari nchini Marekani VIACOM kwa ($340 million) sawa na zaidi ya Tsh. 786 bilioni. Viacom ndio wamiliki wa vituo kama: MTV, Nickelodeon, BET na nyingine kibao.

Pluto TV ilianzishwa mwaka 2013, inapatikana kwenye applications 14. Mpaka sasa ina zaidi ya washirika 75 wakutoa maudhui (content partners), zaidi ya chaneli 100 za bure, na utazamaji wake unafikia zaidi ya watu milioni 6 kwa mwezi.
Loading...

No comments: