KANYE WEST AWASHITAKI TENA JAY Z NA ROC-A-FELLA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

KANYE WEST AWASHITAKI TENA JAY Z NA ROC-A-FELLA


Kanye West aliamkia mahakamani mnamo ijumaa kufungua mashtaka mawili juu ya kupata usawa wa pesa zake, na amewashtaki Roc-A-Fella Records na EMI, kampuni ambayo ilimsaidia kutoboa kwenye muziki.

Mtandao wa TMZ umetanabaisha kuwa Kanye amewashtaki Roc-A-Fella Records ya Jay-Z kwa kile anachodai ni pesa zake pamoja na tamko juu ya stahiki zake baada ya kuwahi kusaini mkataba wa kufanya nao kazi mwaka 2003 pia alishiriki kuipika album ya sita ya Jay-Z 'The Blueprint'

Ye pia amewafungulia shtaka kampuni ya uchapishaji wa muziki na hati miliki EMI akidai pesa zake na tamko la mgawanyo wa stahiki zake baada ya kusaini nao mwaka 2004 na kusajili zaidi ya kazi (nyimbo) 200 alizoandika na kuwaandikia wasanii wakubwa hadi mwaka 2011.
Loading...

No comments: