Kanye West kuburuzwa mahakamani, aponzwa na viatu vyake vya Yeez - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 26, 2019

Kanye West kuburuzwa mahakamani, aponzwa na viatu vyake vya YeezImage result for yeezy kanye west


Rapa Kanye West yupo mbioni kuburuzwa mahakamani kujibu tuhuma za madai ya dola $600,000 sawa na Tsh Bilioni 1.6, baada ya kuzinguana na kampuni ya Toki Sen-I Co.
Kampuni ya Toki Sen-I Co imedai kuwa ndio ilikuwa inamuuzia Kanye West malighafi ya kutengenezea viatu vyake vya Yeezy toka ilipoanzishwa.
Image result for yeezy kanye west

Kampuni hiyo imesema, Kanye aliagiza mzigo wa dola laki 6 lakini baadae alipoletewa mzigo, akasema hanunui tena material kutoka kwao.
Related image
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Kampuni hiyo imesema kuwa walipatana kibiashara na Kanye West mwezi June mwaka jana, na alitaka materials ya dola $624,000 .
Kampuni hiyo inataka fidia ya usafirishaji na mauzo, kwani wamiliki wake wamesema hawana mtu wa kumuuzia material hayo.
Tayari Kampuni hiyo ya inayojishughulisha na masuala ya fasheni ya Toki Sen-I Co. imeshafungua kesi ya madai dhidi ya Kanye West .

No comments: