STAA wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo Jumamosi, Januari 26, 2019 amewakabidhi nguo zake watu walionunua katika zoezi lake la kuuza baadhi ya nguo zake kwaajili ya kukusanya fedha ili kuwezesha project yake ya Save My Valentine, alilolenga kuwasaidia watu wasiojiweza.

Akizungumza wakati wa kukabishi nguo hizo, Lulu amesema kwa leo amekabidhi takribani nguo 36 kati ya 40 ambazo tayari zilikuwa zimeshapata wateja na kwamba mwitikio wa zoezi hilo umekua mzuri na unatia moyo kwa sababu watu wamepokea wazo lake vizuri na kumsapoti.

“Zoezi bado linaendelea, nitaposti tena jumatatu na watu wanaohitaji tutawasiliana ili wanunue. Ninafanya hivi kwa sababu nataka siku moja nikiondoka duniani niache alama ya mazuri niliyofanya, nimefanya mabaya mengi, nimepitia magumu mengi katika maisha yangu, lakini sasa hivi ni wakati wa kufanya angalau mema ili siku moja nikumbukwe kwa hiki ninachiokifanya,” alisema Lulu.
Na Edwin Lindege | GPL
No comments:
Post a Comment