MAREKANI YAISHITAKI KAMPUNI YA SIMU YA CHINA HUAWEI KWA MAKOSA 13 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

MAREKANI YAISHITAKI KAMPUNI YA SIMU YA CHINA HUAWEI KWA MAKOSA 13Taifa la Marekani kupitia Department of Justice imeishtaki kampuni kubwa ya mawasiliano ya nchini China, Huawei pamoja na afisa mkuu wake wa fedha, Meng Wanzhou kwa makosa takribani 13 hapo juzi.

Mashataka hayo ni pamoja na ubadhirifu wa fedha, kupinga utekelezaji wa haki, wizi wa teknolojia nk. Wachambuzi wengi wa maswala ya kisiasa na kidiplomaisa wanasema kesi hiyo huenda ikazua mgogoro wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili ya Marekani na China hali ambayo itaathiri biashara ya kampuni hiyo.

Kampuni ya Huawei imekanusha madai hayo siku ya jana. Katika taarifa yao, Huawei imesema kuwa imeghadhabishwa na mashtaka dhidi yake. Mashtaka hayo yanadai kuwa Huawei iliipotosha Marekani na benki ya kimataifa na kufanya biashara na Iran kupitia kampuni zake mbili za mawasiliano,Huawei Device USA na Skycom Tech.

Kesi ya pili inadai kuwa Huawei iliiba teknolojia, siri za kibiashara pamoja na vifaa kutoka kwa T Mobile katika kufanyia majaribio ya kudumu kwake, pamoja na kupinga sheria na ubadhirifu wa fedha kupitia mtandao.

Department of Justice ya Canada imethibitisha kuwa mahakama kuu ya nchini Canada imepokea mashitaka hayo na kesi inaendelea kusikilizwa.

SOURCE: CTV NEWS
Loading...

No comments: