Mbwana Samatta Alivyowateka Wazungu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 19, 2019

Mbwana Samatta Alivyowateka Wazungu


MBWANA Samatta amezidi kung’ara kwenye vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja. Samatta ambaye anaichezea KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji, ndiye kinara wa wafungaji wa ligi hiyo akiwa ametupia mabao 15 katika michezo 20 aliyocheza.

 Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC na TP Mazembe, sasa thamani yake inatajwa kuwa zaidi ya Sh bil 17 ambapo alitua Genk kwa Bil 1.3 tu mwaka 2016.

 Kazi ya staa huyo mwenye urefu wa futi tano na inchi 11, imemfanya ahusishwe kutakiwa na klabu mbalimbali ikiwemo Everton ya England na nyingine kadhaa. Sasa hebu tucheki baadhi ya timu ambazo zinatajwa kumfukuzia.CARDIFF CITY Cardiff City inayoshiriki Ligi Kuu ya England inapambana kusaka saini ya mshambuliaji ili iweze kuongeza kasi zaidi kwenye ligi.
Loading...

No comments: