MEEK MILL & J.COLE KUTUMBUIZA KATIKA NBA ALL STAR MWAKA HUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

MEEK MILL & J.COLE KUTUMBUIZA KATIKA NBA ALL STAR MWAKA HUUHii ni habari njema kwa wale wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa kikapu hasa wale watakaohudhuria mchezo wa NBA ALL STAR kwa mwaka huu 2019 kwa burudani iliyoandaliwa sio ya kitoto. 

Michezo hiyo ya NBA All-Star Game 2019 itafanyika February 17 katika uwanja wa Spectrum Center mjini Charlotte, nchini Marekani na orodha ya mastaa watakao sherehesha michezo hiyo tayari imewekwa wazi.

Katika List hiyo wapo Rapper J. Cole, Meek Mill na mwanadada Carly Rae Jepsen ambaye ataimba wimbo wa taifa la Canada na Anthony Hamilton akiimba wimbo wa taifa la Marekani.  

Cole anarejea kwenye dimba la All-Star Celebrity Game baada ya kufanya hivyo mwaka 2012. Na itakuwa siku spesho kwa mashabiki wa Meek Mill kumshuhudia akitumbuiza mara baada ya kutoka jela na kuachia albamu yake siku za karibuni. 
Loading...

No comments: