MSAIDIZI WA MOURINHO ATIMKIA QATAR - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, January 23, 2019

MSAIDIZI WA MOURINHO ATIMKIA QATAR


Aliyekuwa kocha msaidizi wa zamani wa Jose Mourinho, Rui Faria amepata kazi ya kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al Duhail ya Ligi ya Qatar Stars. 

Faria alikuwa msaidizi wa Mourinho kwa kipindi cha miaka 17 katika vilabu kadhaa vikubwa Duniani na wameshirikiana katika mafanikio na changamoto zote katika miaka yote hiyo. 

Rui Faria ametambulishwa leo kwenye mkutano na waandishi wa habari akisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu. 

Alipoulizwa kama alimuomba ushauri aliyekuwa bosi wake Jose Mourinho alijibu " Hapana sikuomba ushauri wa Mourinho, huu ulikuwa uamuzi wangu binafsi."
Loading...

No comments: