Msanii mkongwe wa muziki Afrika, Oliver Mtukudzi azikwa kitaifa Zimbabwe, kiongozi wa upinzani atimuliwa msibani (picha) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

Msanii mkongwe wa muziki Afrika, Oliver Mtukudzi azikwa kitaifa Zimbabwe, kiongozi wa upinzani atimuliwa msibani (picha)

Msanii mkongwe wa muziki barani Afrika kutoka nchini Zimbabwe, Oliver Mtukudzi amezikwa kitaifa nchini humo leo Januari 27, 2019 na maelfu ya watu nchini humo.

Pallbearers carry the coffin of the late Zimbabwean jazz and afro pop musician Oliver Mtukudzi as it departs at the National Sports Stadium in Harare,
Mwili wake umeagwa kitaifa katika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, na shughuli hiyo imehuduriwa na maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi hiyo.
Part of the thousands of fans who attended the National Sports Stadium in Harare, Zimbabwe, 26 January 2019.
Mwili wake ukiwa katika uwanja wa taifa wa mpira wa miguu nchini humo siku ya jana Jumamosi Januari 26, 2019, mwili wa Mtukudzi ulisafirishwa kwa Helikopita hadi kijijini kwao nje kidogo ya mji wa Harare nchini humo kwa ajili ya mazishi siku ya leo Jumapili Januari 27, 2019 .
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kiongozi mkubwa wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa alizuliwa kuingia kwenye sherehe za kuuaga mwili wa Mtukudzi.
Mtukudzi katika kipindi cha uhai wake alirekodi album 60 na zote zimefanya vizuri sokoni.
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa alitangaza kuwa msanii huyo ni “Shujaa wa Taifa” mapema siku ya Alhamisi baada ya kifo chake.
Loading...

No comments: