Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James akutana na Mwenyekiti wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Tawi la China Shauku Kihombo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James akutana na Mwenyekiti wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Tawi la China Shauku KihomboTAARIFA YA MKUTANO WA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA NA
MWENYEKITI WA CCM TAWI LA CHINA
Mwenyekiti wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Tawi la China Ndugu Shauku Kihombo
amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati
kuu ya CCM Ndugu Kheri Denice James Leo Jumatatu Januari 21, 2019 Ofisini kwake jijini
Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Ndugu Shauku Kihombo amefikisha salamu za jumla za
Wanachama na Viongozi wa Tawi la CCM China.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Kheri Denice
James ameshukuru kupokea salamu hizo na pia amefurahishwa na diaspora kuendelea kuwa
nguzo muhimu katika ujenzi wa Chama na Taifa.
Komredi Kheri James amesema kuwa TANZANIA inaendelea kupiga hatua za maendeleo kwa
kasi na kusisitiza kuwa kwa pamoja tuendelee kumuombea siha njema Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. John Pombe Joseph
Magufuli kwa kuongoza vyema Taifa letu.
Ndugu Kheri ameongeza kuwa suala la ulinzi na usalama wa watu na mali zao limeendelea
kuimarishwa na ujenzi wa miundombinu bora unaendelea vizuri.
Aidha, Komredi Kheri James amehimiza wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi
kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea na kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kutanguliza
maslahi ya Taifa na Uzalendo.

Victoria Mwanziva
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI
CCM-CHINA

21/01/2019
Loading...

No comments: