NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI APIGA 'STOP' KAMATAKAMATA YA NG'OMBE WANAOZAGAA MTAANI MANISPAA YA TABORA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, January 23, 2019

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI APIGA 'STOP' KAMATAKAMATA YA NG'OMBE WANAOZAGAA MTAANI MANISPAA YA TABORA


 Baadhi ya Mifugo

 Baadhi ya Wafugaji walipokuwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wafanyabiashara wa mifugo katika Mnada wa Ipuli mkoani Tabora jana
 
Na Amisa Mussa

NAIBU Waziri Wa Mifugo Na Uvuvi Abdallah Ulega ameiagiza Serikali ya Mkoa wa Tabora kuitaka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kusitisha mchakato wa ukamataji wa ng'ombe ambao wanadaiwa kuzagaa mitaani baada ya kuonekana kuna harufu ya rushwa.

Mbali ya rushwa katika kuutekeleza mchakato huo imedaiwa linawaumiza wafugaji na wafanyabiashara ya ng'ombe ambao wanafanyabiashara mnada wa Ipuli wilayani humo.

Kutokana na kuwepo kwa gogoro baina ya wafugaji na Halmashauri ya Manispaa Ya Tabora Naibu Waziri Ulega mmetembelea mkoani humo ili kujionea hali halisi ambapo baada ya kusikiliza malalamiko kutoka kwa wafugaji ameamua kutoa maagizo ya kukamatwa kwa watendaji wa halmashauri waliohusika kutekeleza mchakato huo kwani kuna harufu ya rushwa.

Pia ameagiza Ofisa Mifugo Msaidizi Cornelius Masawe akamatwe na hivyo alikamatwa huku akimtaka ofisa hiyo kufanyiwa uchunguzi kwani ndio amekuwa akitekeleza agizo hilo la kukamata ng'ombe ndani ya manispaa hiyo.

Baada ya uamuzi huo Naibu Waziri huyo alipata fursa ya kusikiliza malalamiko ya wafugaji na wafanyabiashara ya ng'ombe ambao hawakusita kpaza uauti zao."Kilichofanyika sasa hivi ni kushika mashavu basi, tunamshukuru Mungu kwa sababu mimi nilikuwa na ng’ombe 45 kwa kumatwa na Masawe zimebaki ng’ombe 13 Nyingine zimeshaliwa,”alisema Alon mmoja wa wafugaji

Wafugaji Emmanuel Cosmas na Jani Kasunzu wamemueleza Naibu Waziri kuwa imefika wakati suala la suala la ng’ombe limekuwa ni dili kwa baadhi ya watumishi.Akiwa katika mnada wa Ipuli Manispaa ya Tabora na kusikiliza kilio cha wafugaji hao Naibu Waziri Ulega ameonesha kuguswa na malalamiko hayo ambapo aliamua kutoa msimamo wa Wizara.

“Ni lazima Oparesheni hii isimame ili iratibiwe vyema na hatimaye baadae ndio iendelea lasivyo tutawadhuru watu ambao hawana hatia,” alisema Naibu Waziri Ulega.

Aidha mwishoni mwa Wiki iliyopita wafugaji na wafanyabiashara wa ng’ombe waliingia katika mgogoro na Halmashauri ya Manispaa Ya Tabora hatua ilyosababisha jamii hiyo ya wafugaji kugoma kutumia mnada wa Ipuli kuuza na kununua ngo’mbe wilayani humo kwa kile kinachodaiwa kamatakamata ambayo imekuwa ikifanywa na Manispaa ya Tabora.
 
Loading...

No comments: