NYOTA HAWA WA SIMBA KUWAKOSA WAARABU WA MISRI


WACHEZAJI wanne wa kikosi cha Simba wataukosa mchezo wa Ligi ya Mabngwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa Februari 2 mwaka huu.

Simba wapo kundi D wanatarajiwa kucheza na Al Ahly ambao kwa sasa ni vinara wa kundi D huku Simba wakiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo miwili wakiwa na pointi tatu.

Imeelezwa kuwa wachezaji hao watakaowakosa waarabu ni pamoja na Muzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na David Mlipili.

Kikosi cha Simba kinawafuata leo waarabu wa Misri huku kikiwa kimebeba matumaini ya kurejea na ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye kundi lao.

Post a Comment

0 Comments