Ole Gunnar afunguka mengi kuhusu Sanchez na kueleza sababu za Fergurson kuwatembelea mazoezini - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, January 2, 2019

Ole Gunnar afunguka mengi kuhusu Sanchez na kueleza sababu za Fergurson kuwatembelea mazoezini


Kocha wa Manchester United Mnorway Ole Gunnar amefunguka mengi kuhusu winga wake raia wa Chile Alex Sanchez.

Kocha huyo amesema kwamba ana matumaini makubwa na winga huyo :- ” Nafikiri ni mmoja wa wachezaji ambao watafaidika sana na mbadilishano na mzunguko wa wachezaji ninaoendelea kuufanya, anauwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za magoli pia ana uwezo wa kufunga nahisi atanifaa sana.Nafikiri ana malengo makubwa sana nimemuona akifunga magoli mengi mazoezini hata siku ya jumamosi katika mazoezi”
Ikumbukwe kwamba Sanchez amekosa michezo takribani tisa iliyopita baada ya kuumia hamstring na hajapata goli lolote kwa karibu miezi mitatu sasa.
Ole Gunnar aliongeza ” Atacheza mchezo wa ligi wa jumatano dhidi ya Newcastle, maana anatamani kucheza kila mchezo na namuona ni mtu anaweza kucheza kila mchezo” Nadhani Rashford atakuwa mzuri, amekuwa akifanya kazi kwa bidii na amechoka sana nafikiri atakuwa mzuri kwa ajili ya Newcastle.”

Lkini pia Solskjaer aliomba msaada wa Sir Alex Ferguson kabla ya kushinda mchezo dhidi ya Bournemouth kwa kumkaribisha bosi wake wa zamani katika viwanja vya mazoezi vya Carrington ili kuangalia mafunzo.
Na kuongeza ” Nimekuwa naye kwa miaka 15,” Solskjaer alisema. “Kwa hakika aliniongoza vizuri zaidi katika miaka 15 hiyo kuliko hiki nilichofanya wiki iliyopita, lakini ninaendelea kumjulisha kila kitu.”
“Yeye alitupa ziara. Alifurahia wakati wake kwenye uwanja wa mafunzo, tulikuwa na mazungumzo mazuri tu na wafanyakazi na alitutia moyo.

“Anajua wafanyakazi ninao nao ni Man United kupitia kwetu, Yeye anajua tutafanya chochote tunaweza, hadi kipindi cha pili tupo hapa, na anajua Man United tutafanya vizuri tuwezavyo.”

No comments: