R. KELLY ANAJIANDAA KUACHIA ALBAMU MPYA KARIBUNI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

R. KELLY ANAJIANDAA KUACHIA ALBAMU MPYA KARIBUNIHabari zilizotufikia punde ni kuwa gwiji wa muziki miondoko ya RnB, Robert Sylvester Kelly, maarufu kama R.KELLY anajipanga kuachia album mpya ambayo itakuwa ni albamu ya 18 katika maisha yake ya kimuziki toka atoe ya kwanza mnamo mwaka 1993. 

Tovuti ya Billboard imeripoti kuwa tayari album hiyo imekamilika na uongozi wake unatafuta kampuni ambayo itaisambaza kwani wiki mbili zilizopita kampuni ya Sony RCA ambao ndio walikuwa wanasimamia kazi zake, walitangaza kumtema kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomuandama. 

Mambo mengi yamemuendea kombo R.Kelly hasa baada ya kuachiwa kwa makala iitwayo "SURVIVING R.KELLY" ambayo inaelezea namna alivyokuwa akiwanyanyasa kingono mabinti wadogo na wasichana kwa ujumla. Makala hiyo iliwarekodi wahanga wa manyanyaso hayo wakielezea jinsi R.kelly alivyokuwa akiwafanyia unyama huo. 

Wasanii wengi akiwemo NE-YO, CELINE DION, nk wamekuwa wakiomba radhi na kutoa mitandaoni kolabo zao walizofanya na R.Kelly ikiwa ni moja ya njia za kupinga ukatili huo wa kijinsia ambao R.Kelly anashutumiwa kuzifanya. 

Je unadhani Albamu hii mpya anayoenda kuiachia bwana R.KELLY itafanya vizuri sokoni?  
Loading...

No comments: