Rais Magufuli amtwisha Waziri Biteko mzigo uliomshinda Kairuki ‘kafunge kamera, ukishindwa ujiandae kuondoka’ (+video) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

Rais Magufuli amtwisha Waziri Biteko mzigo uliomshinda Kairuki ‘kafunge kamera, ukishindwa ujiandae kuondoka’ (+video)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko kufunga Kamera katika ukuta wa madini ya Tanzanite wa Mererani, ndani ya mwezi huu au ajiandae kuachia ofisi yeye na Naibu Waziri wake endapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 22, 2019 wakati akihutubia mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.
“Niliagiza kufungwe Kamera katika ukuta wa Mererani lakini mpaka sasa hazijafungwa, ndio tatizo la Mawaziri wa Tanzania unatoa maagizo hawasikilizi” amesema Rais Magufuli na kutoa agizo.
Nakuagiza tena Waziri Biteko, kafunge kamera ndani ya mwezi huu maana usipofanya hivyo ujiandae kuondoka na Naibu wako na makatibu wako, yaani hadi niondoke na nyie nimewamaliza“.amesema Rais Magufuli.
Loading...

No comments: