RASMI: ANTHONY MARTIAL AMWAGA WINO UPYA MAN UNITED - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

RASMI: ANTHONY MARTIAL AMWAGA WINO UPYA MAN UNITEDManchester, England
Winga machachari wa klabu ya Manchester United (Mashetani wekundu) Anthony Martial, amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Manchester United mpaka ifikapo mwaka 2024 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi. 

Awali mkataba wake ulikuwa unaisha mwisho wa msimu huu na alianza kuhusishwa na kuhamia katika vilabu vikubwa kama Real Madrid, na PSG. 

Maongezi ya mkataba huu yalianza muda mrefu huku Martial pamoja na Agent wake wakikataa ofa kadhaa za united hasa ile ya mwezi Oktoba mwaka jana 2018. 

Baada ya kusaini mkataba juo Martial alisema "Ninapenda muda niliokuwa hapa. Tokea siku ya kwanza kuja wamenifanya nijione mimi ni mmoja wa wanafamilia. Nawashukuru sana mashabiki kwa upendo wao wa ajabu ambao umezidi kunishangaza zaidi na zaidi."
Loading...

No comments: