SABABU ZA KWANINI FC BARCELONA WAMEMSAJILI KEVIN PRINCE BOATENG: - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

SABABU ZA KWANINI FC BARCELONA WAMEMSAJILI KEVIN PRINCE BOATENG:

Catalan, Spain
Mnamo jumatatu ya Tarehe 21/01/2019 usiku, Klabu nguli nchini Hispania na barani Ulaya yenye maskani yake mjini Catalan Hispania, FC BARCELONA ilifanya usajili wa kushangaza na ambao haukutegemewa na mashabiki wa soka duniani kote wa kiungo raia wa GHANA, KEVIN PRINCE BOATENG kwa mkopo wa miezi 6 kutokea klabu ya SASSUOLO inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama SERIE A.

Kutokana na usajili huo kuwa ni wa ghafla na uliofanywa kwa usiri, Watu wengi wamekuwa wakijiuliza KWANINI BOATENG? Na kwanini sasa hivi? Hii ni kwasababu BOATENG ana umri mkubwa kwa sasa wa miaka 31 na Barcelona ilitegemewa itafute vijana wadogo wenye vipaji vikubwa vya soka ulimwenguni. Kingine ni kuwa mashabiki wengi hawaoni kama Boateng ni mmoja wa wachezaji wenye uwezo wa kucheza mifumo na staili za Barcelona.

Tumekuandalia sababu za kwanini FC BARCELONA imeamua kumsajili KEVIN PRINCE BOATENG:

1. UZOEFU: Utakubaliana name kuwa kuchezea timu kubwa kama Barcelona inayoshiriki mashindano makubwa duniani ni lazima uwe na uzoefu wa kucheza timu kubwa au ligi kubwa. Kevin Prince Boateng ana uzoefu huo kwani FC BARCELONA inaenda kuwa timu yake ya 11 kuichezea katika ligi kuu 4 barani ulaya. Timu zingine alizowahi kuchezea ni pamoja na AC MILAN, SASSUOLO, LAS PALMAS, SCHALKE 04, EINTRACHT, HERTHA BSC, PORTSMOUTH, TOTTENHAM HOTSPURS, na BORUSSIA DORTMUND.

2. ANACHEZA NAFASI NYINGI UWANJANI (KIRAKA): Kevin ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, winga wa pande zote mbili, kiungo mchezeshaji/mshambuliaji pamoja na kucheza kama mshambuliaji wa pili (nyuma ya mshambuliaji wa mwisho). Hii ni faida kwa FC BARCELONA.

3. NI MKOPO WA BEI RAHISI: Imewagharimu FC BARCELONA kiasi cha Paundi millioni 1.8 tu za kumlipa mshahara bwana Boateng kwa muda wa miezi 6 na wataweza kumnunua moja kwa moja mwisho wa msimu (kama wakitaka) kwa paundi millioni 8 tu.

4. ATAONGEZA NGUVU KATIKA KIKOSI CHA BARCA: Kama alivyo ARTURO VIDAL, Kevin pia ni mpambanaji uwanjani anayeweza kutumia nguvu na akili na ana uwezo mkubwa wa kutumia miguu yote miwili.

5. BARCELONA KUKOSA OPTION NYINGI KATIKA IDARA YAO YA USHAMBULIAJI: Kwa muda mrefu mashabiki wa Barcelona wamekuwa wakiwaza itakuwaje iwapo MESSI au SUAREZ wakaumia? Nani ataziba pengo kikamilifu? Sasa kwa msimu huu wanataka kombe la klabu bingwa barani Ulaya lakini pia wapo katika mashindano mengine ambayo yanaweza kuwachosha sana wachezaji wao wanaowahitaji mno. So kumleta mtu kama Boateng kunampa kocha option nyingi na kuwapumzisha wale watu muhimu kwa ajili ya mechi za muhimu Zaidi. Isitoshe OUSMANE DEMBELE ameumia pia.


Haya ni machache ambayo tumekuandalia kwa leo. Kama una la kuongezea usisite kuacha comment yako hapo chini.


Loading...

No comments: