SERIKALI YATOA TAMKO BAADA YA SIMBA KUPIGWA 5-0 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, January 20, 2019

SERIKALI YATOA TAMKO BAADA YA SIMBA KUPIGWA 5-0


Kufuatia kichapo cha mabao 5-0 ilichokipata Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema bado hawajakata tamaa.

Makamba ambaye ni shakibi damu wa Simba, anaamini kuwa timu yake itaendelea kujiandaa vema na mechi zijazo ili ije kufanya vizuri.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ambao mara nyingi hupenda zaidi kuutumia, ameandika kuwa kupoteza dhidi ya Vita si mwisho wa safari na haitawakatisha tamaa.


No comments: